Skip to content Skip to sidebar Skip to footer

Je Mfungo Ni Salama Kwa Kila Mtu?

Kila kipindi cha mfungo kinapokaribia, swali moja hujitokeza mara nyingi:

“Je kufunga ni salama kama nina ugonjwa?”

Baadhi ya watu wanaambiwa wasifunge kabisa.Wengine wanafunga bila maandalizi na kupata matatizo.Na wengine wanakosa faida zote za mfungo kwa sababu ya njia wanayotumia.

Ukweli ni huu:
Mfungo siku zote una faida kubwa kwa afya, lakini usalama wake unategemea hali ya mwili na namna unavyoanza.

Tatizo Kubwa Sio Mfungo : Ni Maandalizi

Watu wengi wanaingia mfungo wakiwa na:

  • Mfumo wa chakula mbovu, hivyo kufungulia vyakula visivyofaa.
  • Insulin levels kwenye damu kuwa kubwa, na kufanya wakati wa mfungo njaa kuwa kali mno, kwa maana seli zinazotegemea sukari ni nyingi kwenye mwili(craving receptors)
  • Stress kubwa inayotakana na lifestyle, vyakula vya wanyama na kutokupata muda wakutosha wakupumzika.
  • Mfumo dhaifu wa mmeng’enyo
  • Hormonal imbalances

Halafu wakipata dalili kama kichwa kuuma, kizunguzungu au uchovu, wanaamini mfungo ndio tatizo.Lakini mara nyingi tatizo ni mwili ambao haujaandaliwa. Ni sawa na kuanza mazoezi makali bila maandalizi.

 Mwili Hufanya Nini Wakati wa Mfungo?

Wakati wa mfungo sahihi, mwili hupitia mabadiliko muhimu:

  • Kupunguza matumizi ya insulin na kuondoa hizi craving receptors
  • Mwili huanza kutumia mafuta kama nishati hivyo kusaidia kuondoa mafuta mabya nakupungua.
  • Mfumo wa mmeng’enyo hupata muda wa kupumzika na kujijenga upya.
  • Mwili kuondoa inflammations hasa kwenye mfumo wa mmeng’enyo, kwenye viungo
  • Seli mpya za mwili hujizalisha na viungo kama ini hujizalisha na kujivua gamba kama nyoka.
Mfungo na Magonjwa ya Kisasa

Mabadiliko haya yanaweza kusaidia sana watu wenye matatizo mbali mbali ya kiafya na kuleta uponyaji wa haraka.

1. Kwa Wenye BP(Presha)

Kuupa mwili nguvu ya kujisafisha, kuondoa mucus(mafuta) kwenye njia za mishipa, kufanya moyo na mishipa yake ya kusukuma damu ifanye kazi kwa ufanisi hivyo kudhibiti hili tatizo.

2. Kwa Wenye Kisukari

Kupunguza frequency ya kula kuta kusaidia mwili kuwa active na kuwa sensitive kwenye uzalishaji wa insulin na kupelekea utulivu wa sukari.

3. Kwa Wenye Acid Reflux

Kutokula kipindi cha mfungo mfumo wa mmeng’enyo unajisafisha na kuondoa fermentantion tumboni ambayo ndio inachangia hali ya acid reflux kwa ukubwa. Na kama una vidonda vya tumbo ni kuwa makini na mlo wako wa mwisho na wa kwanza unaofungulia kabla na baada ya kufunga.

Watu Wanaohitaji Tahadhari Zaidi

Muhimu kuelewa: Mfungo si tiba ya haraka, ila unakupa mabadiriko ya kudumu ya afya yako na kukuongezea siku nyingi za kuishi.

  • Mfungo unahitaji usimamizi maalum kwa:
  • Wanaotumia insulin au dawa za kushusha sukari
  • Presha na hawajaanza kufuata njia sahihi za kuitibia bado.
  • Mama wajawazito
  • Watu wenye uzito mdogo sana
  • Watu wenye vidonda vya tumbo visivyotibiwa

Kwa hawa, hatua ya kwanza ni kutibia magonjwa au kurekebisha chakula na mfumo wa maisha kabla ya kuanza mfungo mrefu.

Kanuni 3 za Mfungo Salama
  1.  Andaa mwili kusafisha tumbo(Piga bomba)na safisha viungo vyako.
  2. Anza polepole, kwa mtu anayeanza kabisa anaweza fanya mfungo wa matunda, kisha mfungo wa maji tu, mpaka kuanza kufunga kavu.
  3. Fungua kwa utaratibu na vyakula vya asili. Unaweza fungua na herbal tea au uji wa mtama mweupe, nazi na tende zako, usitumie ngano, sukari au vitu visivyo faa muda wa kufungulia.

Ukifuata kanuni hizi, mfungo huwa zana ya kurekebisha mwili, sio chanzo cha mateso.

Hitimisho

 Mfungo sio hatari kwa kila mtu. Na sio suluhisho la kila kitu. Ni njia ya uhakika yenye nguvu, lakini inahitaji uelewa. Badala ya kuogopa mfungo, jifunze kuutumia kwa usahihi kulingana na hali ya afya yako.

Kama una BP, kisukari au acid reflux na unataka kujua namna salama ya kufunga kulingana na hali yako binafsi,

Wasiliana nasi kwa ushauri. Namba zetu ni 0746956774 au 0754501193, pia tembelea page zetu Instagram, Youtube au Tiktok kwa jina la Praxeda Makanshu au LIFE REVIVAL HOME THERAPY.

Na kama makala hii imekusaidia, ishiriki na mtu anayehitaji mwongozo sahihi kuhusu mfungo na afya.

Leave a comment

0.0/5